Wednesday, October 9, 2013

Justin Timberlake na Robin Thicke kutumbuiza kwenye harusi ya Pharell Williams?

Justin Timberlake na Robin Thicke wanadaiwa kuwa watatumbuiza kwenye sherehe ya harusi ya Pharell Willliams Jumamosi hii.
Pharrell-Williams-and-Helen-getting-married1
Producer huyo mwenye miaka 40 anadaiwa kuwaomba wanamuziki
hao ambao wote ameshawatengeneza nyimbo ukiwemo wimbo wa Robin Thicke, Blurred Lines. Pharrell na mke wake Helen Lasichanh watafanya sherehe hiyo huko Miami.
Helen Lasichanah ni designer na model na wamezaa na Pharrell mtoto mmoja aitwaye Rocket. Mwezi August mwaka huu walifunga ndoa kimyakimya nchini Ufaransa.
“Pharrell amefanya kazi na kila mtu. Ametayarisha albam ya Miley Cyrus, amefanya kazi na BeyoncĂ©, Madonna, Shakira, Daft Punk, Kanye West na Jennifer Lopez. Nusu ya tasnia ya muziki itakuwa pale,” kilisema chanzo kimoja.


No comments:

Post a Comment

ShareThis