Thursday, October 3, 2013

Nay wa Mitego kuachia remix ya Salam Zao aliyowashirikisha zaidi ya wasanii sita

Nay wa Mitego amesema mashabiki wake wakae mkao wa kula kusikia remix ya Salam Zao ambayo wasanii zaidi ya sita watadondosha bars zao.



Akiongea na Kali za Bomba ya Bomba FM, Mbeya Nay wa Mitego amesema ameamua kufanya remix ili kuwapa fursa wasanii wengine kusema yale wanaliyonayo moyoni.
“Ukishafanya wimbo mkubwa, lazima uwape nafasi na watu ya kufanya kitu kwenye kile ulichokifanya halafu kila mtu azungumze kile ambacho na yeye labda anatamani azungumze,”alisema Nay.
Pia Nay amesema video ya Salam Zao itatoka hivi karibuni na imefanywa na kampuni ya Empty Souls Production.


No comments:

Post a Comment

ShareThis