Wednesday, October 9, 2013

Picha:je Hii ni njia mpya ya kuadhibu wanaume vicheche? China Style

Unaukumbuka wimbo wa Bushoke ‘Mume bwege’? Laiti kama kijana huyo wa China angekuwa anaufahamu basi wimbo huo ungetawala kichwa chake siku hiyo. Tukio hilo limetokea huko Hong Kong, China baada ya msichana aitwaye Cheng kumtuhumu mpenzi wake Chui kuwa anamcheat.
China bf-3

Kilichomtokea kijana huyo ni kwamba girlfriend wake alimfuma akiwa anampeleka msichana mwingine nyumbani hivyo binti huyo akaamua kuchukua maamuzi ya kumuadhibu boyfriend wake hadharani kwa kumwambia apige magoti njiani mtaani na kumpiga vibao.
china bf-4
Kama unavyojua vita ya panzi furaha kwa kunguru, ugomvi huo ulizipa kazi camera za simu za wapita njia walioamua kujirekodia scene za bure na kupost youtube.
China bf-2
Baada ya tukio hilo polisi walipigiwa simu na msichana huyo aitwaye Cheng (20) alikamatw kwa kosa la kumshambulia na boyfriend wake aitwaye Chui (23) alipelekwa hospitali.
Video ya tukio hilo ilitazamwa zaidi ya mara 700,000 ndani ya siku 3 toka imewekwa. Itazame Hapa


No comments:

Post a Comment

ShareThis