Monday, November 4, 2013

Audio: Master Jay adai wimbo wa Usher ‘Yeah’ ndio ulimfanya astaafu, asema hawezi kurudi na kushindana na maproducer vijana sababu hataki kujiaibisha kama Legendary

Producer mkongwe katika game ya Bongo fleva Joachim Kimario aka Master Jay wa MJ Records amekiri kuwa mabadiliko ya soko la muziki kwa miaka ya sasa ni kati ya sababu zilizomfanya astaafu, sababu anajiona hana uwezo wa kukidhi mahitaji ya soko la sasa, hawezi kushindana na maproducer vijana ambao ndio wameushika muziki wa bongo kwasasa.
Master-J
“unajua tuseme …kama mimi saizi nirudi kwenye muziki sitaweza kushindana na kina Marco Chali na akina Pancho na
kadhalika, mwisho wa siku unakuja kuwa nominated kwenye KILI unakuja kushika mkia si unajiaibisha tu, kila kitu kina wakati wake inafika sehemu unaacha watu wengine wanaendelea ”, Master Jay alifunguka katika mahojiano na King Davidy wa UPLANDS FM ya Njombe jana.
Ni wazi kuwa Master Jay ni mmoja kati ya maproducer wa zamani ambao watu wengi wanatamani kusikia wakiendelea kutengeneza muziki katika kizazi cha hivi sasa, ambacho kimekuwa na changamoto nyingi kwa maproducer kutokana na jinsi muziki unavyozidi kukua na kubadilika.
Master Jay ameamua kuwa muwazi na mkweli kuhusiana na sababu za kuacha kuproduce muziki na kumpa nafasi Marco Chali kuendeleza jahazi la MJ Records
“ Unajua soko limebadilika sasahivi, mi nimeanza muziki naona sasa hivi ni miaka 18 iliyopita, sasa ilifikla sehemu hapa katikati, unajua hili ni soko aah wanakuja vijana wapya aah wanataka ladha tofauti kwahiyo mimi Niko tofauti na hii ladha ya sasa hivi, ndio maana niliamua kustaafu, kwasababu ilifika sehemu niliona kabisa kwamba sehemu ambayo soko linaenda kimuziki sio mimi, kwasababu muziki ni expression ya, wanasema personality ya producer , ni feeling zako sasa feeling zangu haziendani na sehemu ambayo muziki ulikuwa unaenda “ Alisema Jay.
Jay ambaye ndiye muanzilishi na mmiliki wa studio ya MJ Records amekisema kitu ambacho kilikuwa chanzo kikubwa cha yeye kuamua kustaafu kabisa kufanya muziki: “Na nakumbuka kabisa ilikuwa kipindi kile Usher alivyotoa ule wimbo wake ‘Yeah’ yaani ule wimbo ndio ulinifanya mimi nistaafu, wewe ndio ntakwambia leo ukweli, sasa kama ukishaona soko linaenda sehemu ambayo sio wewe huwezi kuforce kitu kwasababu mashabiki wanajua kama mtu anafake kitu watajua tu, kwahiyo kama imeshindikana basi imeshindikana ndio maana mi nikasema ngoja niache, ndio maana nikamtafuta kijana ambaye yeye anaelewa hilo soko na feeling zake na atafanya vizuri ambaye ndio alikuwa Marco Chali ndio maana niko naye mpaka leo”.
Zamani ya Q Chief na Lady Jay Dee ni moja ya nyimbo alizotengeneza Master Jay miaka ya nyuma
Jay amesema kuamua kustaafu haikuwa kazi rahisi kwake sababu tayari alikuwa ameshajenga brand ya MJ Records na watu walikuwa wanajua wanapoenda MJ wanaenda kufanyiwa kazi na yeye, hivyo haikuwa kazi rahisi kuamua kumpa kijiti Marco Chali aendeleze jahazi aliloliongoza na kulijengea jina na sifa kwa zaidi ya miaka 10.
“Unajua inataka moyo kusema kweli , aah sijawahi kuzungumzia hicho kipindi kilikuwa kigumu sana kwangu mimi, unajua umeshazoea kwamaba MJ Records ni Master Jay, aah Psychologically sisi kama binadamu wewe ukishazoea kuwa ndo unasifa zote halafu inabidi urudi nyuma halafu mtu mwingine anachukua hizo sifa unajua nafsi zetu zilivyo, kilikuwa ni kitu kigumu sana roho iliniuma yaani kuna mashetani kichwani ilibidi nifight nao sana, mpaka sasa hivi roho yangu iko safi kabisa yaani niko fresh kwamba MJ Records ni Marco Chali.
Sasa ndio hiyo stage ni rahisi kutamka lakini kufanya ni kitu kigumu sana kwamba mimi nimeanzisha hii kampuni inafika sehemu mtu mwingine ndo anachukua sifa zote ndio maana watu wengi wanaona ni kazi, lakini inabidi ufanye kwasababu uking’a ng’ania sana wakati hauwezi …utakuja tu kujiaibisha kama legendary.”
Jay aliulizwa kama anafikiri hizo sababu za yeye kustaafu ndicho kinamkuta producer mkongwe mwenzake P-Funk wa Bongo Records, hiki ndicho nalichojibu:
“Anakazi , anakazi unajua ni mkali, unajua sio kwamba mtu unakuwa umepungua kuwa mkali, ni kwamba tu soko limebadilika vijana wa sasahivi ni tofauti na wale vijana wa kipindi kile tuliokuwa tunawatengenezea muziki, sasa kama huwezi kutengeneza kitu ambacho wao wanataka huwezi kuwa force wakubali kitu ambacho wa zamani walikuwa wanakikubali…
Master Jay amesema kwasasa japokuwa hatengenezi muziki lakini amekuwa akiendelea kufanya ‘sound engineering ‘ kwa wasanii walio chini yake tu,
“Kitu ambacho mimi nimebaki kuwa nafanya sasahivi MJ Records ni kama Hermy B kamuachia Pancho, unajua kitu ambacho hakibadiliki miaka nenda rudi imekuja miziki ya 80, 90, 2000 mpaka tunakoenda mbele sound engineer ataendelea kuwa sound engineer na ni kitu lazima usomee. Watu watakuja watatengeneza beat kila siku vijana wanatengezea beat kila siku lakini hawajui kurekodi sauti vizuri hawajui kufanya editing hawajui kufanya mixing hawajui kufanya mastering, hivyo ndio vitu ambavyo P-Funk ni mtaalam Bony ni mtaalam mimi ni mtaalam Hermy B ni mtaalam”.
Kuhusiana swala la management ya wasanii Master Jay amesema kuwa wasanii ambao mpaka sasa bado wako chini yake ni Izzo B, Quick Racka pamoja na Shaa na kuongeza kuwa hao ndio ambao huwa anafanya sound engineering katika kazi zao mpaka sasa.
“Kama Shaa nyimbo zake zote hata hii ‘Sugua Gaga’ sauti zote nimerekodi mimi, yaani kupanga sauti kuzirekodi, editing kila kitu ni mimi, Shirko amepiga muziki, kwahiyo mi nawafanyia tu hawa wasanii wangu lakini mtu wa nje itakuwa ngumu kwasababu mi sichaji…lakini nikisema nimchaji mtu aah ntamchaji shilingi ngapi rafiki yangu itakuwa hela nyingi sana, ni kama Hermy B anavyofanya anamix kazi za studio kwasababu anajua zinamuingizia hela”.
Wimbo mpya wa Shaa ‘Sugua Gaga’ ambao Master Jay amesimamia vocals, mixing pamoja na mastering
Msikilize hapa Master Jay

No comments:

Post a Comment

ShareThis