Friday, November 15, 2013

Fahamu idadi ya Tuzo anazomiliki Msanii AY za kitaifa na kimataifa.


Msanii wa muziki na mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa nchini, Ambwene Yesaya aka AY ameweka wazi kuwa tangu safari yake ya muziki ilipoanza mpaka leo, ameweza kujinyakulia tuzo za kitaifa na kimataifa 18 huku mwaka huu pia akitajwa kuwani tuzo za CHOAMVA.

Akizungumza na E-Newz ya EATV, AY alisema ingawa amekuwa mwenye

mafanikio makubwa anawashukuru Watanzania kwa kuweza kumfikisha hapo alipo na hivyo amewataka waendelee kumuonyesha ushirikiano wa kutosha ili kusaidia kufikisha mbali zaidi harakati zake za kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa kupitia muziki.
AY anawania vipngele viwili kwenye tuzo za CHOAMVA 2013 ambavyo ni Video Bora kutoka Afrika Mashariki pamoja na Video Bora ya msanii wa kiume.
Jumapili hii atakuwa na show ya Road to CHOAMVA 2013 kwenye ukumbi wa Club Billicanas jijini Dar.


No comments:

Post a Comment

ShareThis