Friday, November 15, 2013

Prezzo: Huddah ni ‘mali ya serikali’, amelala na karibu dunia nzima


Baada ya kupondwa na Huddah Monroe kuwa ‘amepigika’ mfalme wa bling, Rapcellency Prezzo ameamua kujibu mashambulizi na kusema uhusiano wake na Huddah ulikuwa wa kufanya mapenzi tu, basi.
641028c24b4d11e3993a0ea3ad99e4fd_8
Kwenye interview na Heads Up, Prezzo aliweka wazi kuwa ni kweli aliwahi kuwa na uhusiano wa muda mfupi na aliyekuwa
mwakilishi huyo wa Kenya kwenye Big Brother Africa mwaka huu.
“Tuliwahi kukutana kama mara tatu hivi nadhani alipenda alichokipata. Alinogewa,” Prezzo aliimbia Heads Up.
Anadai kuwa Huddah amechukia kwasababu hakutaka kuendelea naye.
“Huddah ni kama mali ya serikali. Amelala na karibu dunia nzima. Unadhani rais anaweza kutulia na mwanamke kama huyo,”alihoji Prezzo. Alidai pia kuwa Huddah amekuwa akiwasumbua wanawake wote wengine aliowahi kuwa na uhusiano nao.
“Sijawahi kumjibu, lakini utagundua kuwa alimshambulia Goldie na Diva wa Tanzania.”
Wakati huo huo, Huddah amekuwa akitweet majibu ya kile alichokisema Prezzo.


No comments:

Post a Comment

ShareThis