Friday, November 15, 2013

R.Kelly athibitisha kufanya collabo na Justin Bieber, wimbo huo kutoka wiki ijayo


Mashabiki wa mfalme wa R&B R.Kelly na mashabiki wa Justin Bieber watarajie kupata collabo kati ya wakali hao, inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.
Justin n R.kelly
Justin Bieber na R.Kelly
Robert Kelly amethibitisha juu ya collabo hiyo baada ya kuwepo kwa uvumi juu ya
wawili hao kutoa wimbo wa pamoja, uvumi ulioanza kuenea wiki mbili zilizopita.
“I just did a song [with him], [Justin] just called me to do a song and it’s hot. He wanted to go and do some R&B stuff so we got together and did that.” R.Kelly ameiambia VIBE wiki hii wakati wa party binafsi ya kusikiliza albam yake mpya ‘Black Panties’ inayotarajiwa kutoka (December 10) mwaka huu.
Kupitia twitter Justin Bieber pia amethibitisha kuwa wimbo huo alioshirikiana na R.Kelly unatarajiwa kutoka mapema wiki ijayo.


No comments:

Post a Comment

ShareThis