Saturday, November 16, 2013

Mwana FA azungumza na VOA kuhusu hadhi ya muziki wa Bongo na changamoto zake


Hamis Mwinjuma aka MwanaFA amehojiwa na Sauti ya Amerika idhaa ya Kiswahili na akafunguka kuhusu muziki wa Tanzania kushindwa kuendelea na wasanii kunufaika kwasababu mfumo wa muziki wa Tanzania haupo kibiashara.
MWANAFA-NEW
Mwana FA alisema anafikiri muziki wa Tanzania hautaweza kuwanufaisha wasanii mpaka
ifike mahali watu wafanye muziki kiofisi na sio kienyeji.
“Nafikiri upande mmoja,unajua muziki ambao tunaoufanya una pande mbili na upande mmoja ni suala la muziki wenyewe na upande wa pili ni biashara ya muziki. Kwahiyo nafikiri sehemu ambayo ina matatizo bado ni biashara ya muziki.Kitu ambacho nafikiri ambacho kinatukwamisha ni hakujakuwa na hela za kutosha ‘serious money’ kwenye muziki,” alisema FA ambaye kwa yupo jijini Washington DC, Marekani.
“Kwa mimi jinsi ninavyofikiri mawazo yangu lakini,hela za kutosha zitatengeneza mfumo, hakuna mtu atatengeneza milioni mia mbili hamsini ‘250’ kwa mwaka kwenye kampuni halafu akafanya biashara kienyeji,lazima watakuwa na watu wa PA,atakuwa na managers atakuwa na nini, yaani nadhani hiyo itarasimisha moja kwa moja na watu watakuwa wanafanya kazi kama wafanyabiashara moja kwa moja,” aliongeza.
“Unajua kuna studio kila mtaa,mtu ana studio sebuleni kwake,anaweza kutengeza wimbo, akapeleka kwenye radio ukapigwa ,ukawa number 1 hit,ushafahamu? Huyu mtu hajajiandaa hata namna ambavyo anataka kufanya biashara anakuyumbisha. Kwamfano Diamond atakuja atadai show yake anataka kulipwa milioni 8, lakini huyu aliyetengeneza nyimbo yake sebuleni akilipwa laki 3 atafanya hiyo show,kwahiyo inakuwa ngumu. Lakini kungekuwa na utaratibu,kama nafikiria kuhusu ‘record label’ nafikiria jinsi makampuni yataweza kuwalipa wasanii kupitia ‘management’ zao moja kwa moja. Kwahiyo watu nyimbo hazitapigwa,pengine ni ubepari lakini wimbo hautakuwa unapigwa hovyo hovyo. Mpaka kuwe na utaratibu fulani umepitia, means hata watu hao wakipata hela nyingi nini anakuwa amejiandaa. Baada ya hapo kila kitu kinafanyika kiufundi, professional na muziki utapiga hatua.
Tuna soko kubwa sana, kuna WaTAnzania takribani milioni 45, ukiwauzia asilimia moja tu ya Watanzania ukapata elfu moja 1,000 tu kwa kila mtu,bado ni hela nyingi sana ,lakini nafikiri hatutafika hatua hiyo mpaka tufike mahali kwamba watu wafanye vitu kiofisi na sio kienyeji kama tunavyofanya sasa hivi. Kwahiyo nafikiri mahali tunapokwama ni kwenye kuufanya muziki uwe na utaratibu na mfumo ambao unaeleweka ‘mfumo wa kibiashara’ mtanisamehe mimi naamini kuna ubepari kwenye muziki moja kwa moja.
FA pia alisema vijana wengi sasa hivi wanafanya muziki ili uwapatie pesa tofauti na zamani ambapo wao ilikuwa ni ‘passion’.
“Wakati naanza kuimba sikuamini kama waweza kunipatia shilingi elfu 20,ilitokea nafanya kitu ambacho nakipenda,jamaa zangu Tanga Schools wananishangilia na rap kwenye basketball wakati tunacheza wananishangilia basi naenjoy. Kwahiyo ulikiwa unahusiana na vipaji, skills moja kwa moja. Sasa hivi watu wameshajua ni biashara,kila mtu anataka kuwa kama AlI Kiba,kila mtu anataka kuwa Mr Blue,kwasababu ya hela na umaarufu ndio maana inakuwa ngumu,” alisema FA.


No comments:

Post a Comment

ShareThis