Monday, November 11, 2013

Picha: Hatimaye Diamond Platnumz awasili Lagos, Nigeria kwaajili ya kufanya kazi na Davido pamoja na Iyanya


Diamond hakutania aliposema muda si mrefu ataelekea Nigeria kwakina ‘oga’ kwaajili ya kumalizia kile alichokianza na star wa nchi hiyo Davido alipokuja kutumbuiza katika Fiesta siku chache zilizopita.
Diamond Nigeria-3“Naija! we are in Town Baby!!!!…. #Lagos #Nigeria #WCB #wasafi”
Katika moja ya picha alizopost baada ya kutua Naija, inamwonesha msafi akiwa
amevaa t-shirt nyeupe ya Born to shine brand ya B-Dozen wa Clouds FM, huku akiwa ameambatana na watu watatu akiwemo Babu Tale.
Diamond Nigeria-2
“Oooh! Nigerians… your Kindness make me feel like am at Home… #WCB #wasafi #Cocaboys for Life mumy…!” Hii ni caption aliyoiandika katika picha hii
Yawezekana hapa ndipo alipofikia Diamond nchini Nigeria
diamond naija
Katika picha hii aliandika “Back from the Gym na Energy za Kutosha, Lol!….#MyHome #Lagos #Nigeria #WCB #Wasafi for life..!”
Siku chache zilizopita baada ya show ya Fiesta Dar Diamond alirekodi remix ya hit single yake ‘My Number 1’ aliyomshirikisha Davido, na baada ya zoezi la kufanya video ya wimbo huo kushindikana kufanyika Dar es salaam, Platnumz aliahidi kwenda Nigeria kumalizia zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment

ShareThis