Saturday, November 30, 2013

Quick Rocka aomba radhi kwa kutoachia ‘Maasai’ aliyomshirikisha AY baada ya computer ku ‘crash’ na wimbo kufutika

Quick Rocka amewaomba radhi mashabiki wake kwa kushindwa kuachia wimbo wake mpya ‘Maasai’ aliomshirikisha AY baada ya computer ya studio ulipofanyika wimbo huo ku’crash na wimbo huo uliokuwa umekamilika kupotea.
Quick Rocka
Quick alikuwa amepanga kuachia wimbo huo November 28.
Ameongea kuwa itamlazimu kurudia tena kuingiza sauti za
wimbo huo upya.
“Me naanza zangu next week then namsubiri AY akirudi afanye zake. Just waiting for MJ amalize EBSS finals,” amesema Quick.
“I apologise to my dear fans. Hii ilikuwa nje ya uwezo wangu. But as soon as tukimaliza kufanya upya vocals Maasai will be banging your speakers na utaruka kama mori imepanda. Switcher na AY ni collabo ya moto sana, haijawahi tokea.”


No comments:

Post a Comment

ShareThis