Saturday, November 30, 2013

Rick Ross kushirikishwa katika Remix ya wimbo wa Lady Gaga na R.Kelly ‘Do What U Want’


Mwimbaji anayesifika kwa kuteka vichwa vya habari katika mitandao kwa vituko hasa vya mavazi ya ajabu, Lady Gaga, anatarajia kumuongeza staa mwingine wa Hip Hop katika remix ya wimbo wake ‘Do What You Want’.
Rick
Boss wa MayBach Music Rick Ross, anatarajiwa kuungana na R.Kelly na Lady Gaga katika remix hiyo. Gaga amethibitisha kupitia
twitter.
Kelly n gaga2
R.Kelly na Lady Gaga
Lady Gaga na R.Kelly ni miongoni mwa mastaa waliowasuprise watu kwa show ya kiubunifu zaidi, wakati wa tuzo za Marekani (AMA 2013) zilizofanyika wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment

ShareThis