Monday, December 30, 2013

Lamar akerwa na maproducer wanaokopi na kupesti midundo


Producer maarufu anayemiliki studio ya FishCrab, Lamar amesema muziki wa Bongo Flava unapoteza muelekeo kutokana na watayarishaji wa muziki nchini kuigana.
Lamar-1

Akizungumza na enewz ya EATV Lamar amesema kwa muda mrefu amekuwa akikerwa na maprodyuza mbalimbali wasiojituma zaidi ya kukopi na kupaste kazi za wenzao.
Lamar ametoa mfano wa jinsi watayarishaji wengine wanavyoiga beats za nyimbo za Diamond na kuanza kuzitumia kwa manufaa yao binafsi kiasi cha kuchangia kupoteza ladha ya muziki wa Bongo Flava.



No comments:

Post a Comment

ShareThis