Thursday, January 30, 2014

Beyonce Atupiwa lawama na wazazi kwa show yake ya Grammy, wadai ilikua haifai kutazamwa na watoto


Beyonce na Jay Z ndiyo gumzo kwa sasa katika mitandao kutokana na show yao wakati wa tuzo za Grammy zilizofanyika Jumapili iliyopita huko Los Angeles, Marekani.
Bey7
Pamoja na kuwasurprise watu wengi kwa show ya ‘Drunk In Love’ aliyoifanya Beyonce na Jay Z wakati wa tuzo hizo, lakini amepokea lawama nyingi kutoka kwa wazazi waliodai
hawakuwa huru kuwaacha watoto wao watazame tuzo hizo kwenye TV sababu ya kivazi alichokivaa pamoja na uchezaji uliokuwa haufai kutazamwa na watoto.
bey2
bey3
Wazazi wengi wameelezea malalamiko yao kupitia twitter wakidai kuwa, Bey (32) ni mama wa mtoto mmoja na ni mke wa mtu hivyo hakustaili kuvaa kivazi kama kile na kufanya ‘raunchy’ show katika tukio ambalo lilikua likirushwa moja kwa moja kwenye TV.
bey1
Katika tuzo hizo Beyonce ndiye aliyefungua show kwa kuperform hit song yake ‘Drunk In Love’ ambayo amemshirikisha mume wake Jay Z. Hizi ni baadhi ya tweets za malalmiko,
bey tweets
bey5
Kwa sasa video ya show ya Beyonce na Jay Z wakati wa tuzo za Grammy imeondolewa youtube, na huu ndio ujumbe unaotokea ukitaka kuitazama,
‘This video contains content from Grammys, who has blocked it on copyrights grounds’


No comments:

Post a Comment

ShareThis