Thursday, January 30, 2014

Grammy: Macklemore adai Kendrick Lamar alistahili kushinda tuzo ya album bora ya rap na si yeye


Baada ya kushinda vipengele vinne kwenye tuzo za 56 za Grammy zilizofanyika Jumapili jijini Los Angeles, rapper wa Seattle, Ben Haggerty — anayejulikana zaidi kwa jina la Mackle­more — alimwandikia ujumbe Kendrick Lamar na kumweleza kuwa alistahili kushinda tuzo ya album bora ya rap na sio yeye.
page
Album yake “The Heist,” ilishinda na kuzipiku album za
Kendrick Lamar, Drake, Jay Z na Kanye West.
Baada ya tuzo hizo, Macklemore alimtumia Kendrick Lamar ujumbe huu:
cd88e786871a11e39972121de7c604a9_8
Aliuelezea zaidi ujumbe huo kwenye Instagram:
My text to Kendrick after the show. He deserved best rap album… I’m honored and completely blown away to win anything much less 4 Grammys. But in that category, he should have won IMO. And that’s taking nothing away from The Heist. Just giving GKMC it’s proper respect.. With that being said, thank you to the fans. You’re the reason we were on that stage tonight. And to play Same Love on that platform was a career highlight. The greatest honor of all. That’s what this is about. Progress and art. Thank you. #grammys


No comments:

Post a Comment

ShareThis