Thursday, January 16, 2014

King Majuto asaini mkataba mnono na Steps, kutofanya filamu za kushirikishwa tena


Muigizaji mkongwe wa vichekesho, King Majuto ameingia mkabata mpya na kampuni ya usambazaji wa filamu nchini Steps Entertainment ambao hautamruhusu kuonekana kwenye filamu za kushirikishwa.
KingMajuto
Akizungumza  leo mtoto wa King Majuto, Hamza Majuto ambaye pia ni meneja wake,amesema kwa sasa baba yake haonekana kwenye
filamu za kushirikishwa bali ataonekana kwenye filamu zake mwenyewe.
“Unajua Mzee Majuto amefanya filamu nyingi sana za kushirikishwa hali ambayo hajanufaika na chochote,tukaona tuingine mkataba na Steps Entertainment ambao hautamruhusu Mzee Majuto kufanya filamu za kushirikishwa, hata kama mtu aje na milioni 100 haitawezekana. Kwahiyo Majuto atakuwa anafanya filamu zake pekee,ukimuona majuto kwenye filamu ujue ni yake,” amesema Hamza.

“Toka zamani Mzee Majuto alikuwa na mkataba wa kazi na Steps ila huu ambao ameingia na Steps kwa sasa utakuwa unamnufaisha mara mbili ya ule wa zamani. Pia ataonekana mara kwa mara hali ambayo itamfanya awepo sokoni kwa muda mrefu. Kwahiyo mkataba utakuwa na manufaa makubwa sana kwa Mzee Majuto na sanaa yake.”
Hata hivyo Hamza alisema Majuto anaweza kufanya matangazo yoyote ya biashara isipokuwa ya unga kwakuwa ni balozi wa Azam.

No comments:

Post a Comment

ShareThis