Thursday, January 16, 2014

Linex adai nyimbo za harusi zitamtajirisha, aanza kupata booking za kutosha.


Hitmaker wa Kimugina, Linex Sunday aka Mjeda, amesema baada ya kutangaza biashara yake ya kutunga nyimbo za maharusi, ameanza kupata booking lukuki.

Hii dili yangu nakuja kuwa tajiri kabisa hapa mjini,” Linex alisema. “Kwasababu ni big deal na ni deal fulani ambayo nimejaribu ku
google lakini sioni kama kuna msanii amewahi kufanya dunia hii. Kwahiyo nahisi kama Mungu kanipa idea kwenye kichwa changu ili niitumie, it’s a big thing,ni kitu ambacho nakiheshimu sana kwasababu ni kikubwa,mpaka sasa hivi nataka kwenda kuisajiri idea ili asitokee mtu akatumia kaujanja fulani.”“Siwezi sema watu wangapi wameweka booking lakini ni wengi sana, kwahiyo nashindwa kuanza kutunga kwasababu naanda mkataba maalum utakaowabana wateja wangu wasije wakatumia kibiashara nyimbo ninazowatungia.”
linexx




No comments:

Post a Comment

ShareThis