Wednesday, January 15, 2014

Nay wa Mitego kuachia collabo 3 mwaka huu ikiwemo na Nay Lee na Diamond


Hit maker wa ‘Nakula Ujana’ Nay wa Mitego amesema mwaka huu ana collabo 3 ambapo moja ameanza na kufanya na mwanadada NeyLee katika wimbo‘Usinikatae’ utakaotoka hivi karibuni.

“Nimeanza kurekodi ngoma mpya na Ney Lee nikagundua kumbe ni demu fulani ambae anaweza sana halafu kama hana msaada hivi,” Nay amesema “Kwahiyo baada ya kuona uwezo wake katika
wimbo ambao nimefanya naye (Usinikatae) nimeamua kumpa tafu na nitajitahidi kumpushi kidogo kwa namna yoyote kwasababu mimi kidogo nipo mbele yake. KwaHiyo nadhani hivi karibuni ngoma itakuwa inatoka. Hii ngoma ni kali sana,” ameongeza rapper huyo.

“Ney Lee ni msanii ambaye anasimamiwa na watu na mimi namsimamia katika huu wimbo pekee, kwasasabu namchukulia kama dada yangu, alikotokea na alikotokea mama yangu ni kumoja,pia anaweza sana,kwa watu ambao wanamsaidia wataendelea kumsaidia, kila mtu atasaidia kwa nafasi yake. Nimeshaanza kuongea na directors wa video kwasababu hii ngoma siyo ya kuiacha pekee bila video hata baada ya kumaliza kurekodia watu wa studio wakaanza kusema ‘acheni iende kwanza’ ila sisi tukaona bora tusubirie tujue director wa video atasemaje then tutajua tuiachie ama vipi.”

Kuhusu collabo na Diamond, Nay amesema bado hajajua ni ngoma ipi atakayoitoa. “Kuna nyimbo 3 ambazo nimefanya na
Diamond, kwahiyo tunaweza tukaiachia au lah, kwasababu tunataka ikija iwe na video full, vyote vinawezekana.”

No comments:

Post a Comment

ShareThis