Tuesday, March 18, 2014

Baada ya Milolongo yote hatimaye Chris Brown kukaa jela mwezi mmoja hadi April 23


Maisha ya Chris Brown yanaendelea kuandamwa na mikasa kila kukicha kutokana na kushindwa kufata masharti anayopewa hasa katika kipindi hiki ambacho macho ya mahakama yanafuatilia mienendo yake. Baada ya kufukuzwa rehab ijumaa iliyopita sasa mahakama imemuamuru akae jela mwezi mmoja.
Chris+Brown+Chris+Brown+Arrives+Court+Hearing+XDb4-53BO3Al
Kwa uamuzi huo wa mahakama Brown sasa atakaa jela hadi April 23.

Kwa mujibu wa TMZ, sababu zilizopelekea Brown kufukuzwa rehab ni kukiuka kufata sheria na taratibu alizowekewa, moja wapo ikiwa alionekana akimshika mwanamke wa rehab kiwiko na mikono. Moja ya sheria za rehab hiyo kwa Chris ni kukaa umbali wa futi 6 na kila mwanamke wa hapo.
Pia inadaiwa kuwa sababu nyingine amekuwa akikataa kuchukuliwa vipimo vya matumizi ya dawa za kulevya.

No comments:

Post a Comment

ShareThis