Friday, April 11, 2014

Kuhusu taarifa za msanii Shetta kupata ajali ya gari.


Screen Shot 2014-04-11 at 8.55.37 PM
Screen Shot 2014-04-11 at 8.56.21 PM
Kabla ya hii ajali Shetta alinipigia simu saa kadhaa kabla na
kuniambia hii show aliyoitiwa kuna mtu alishakula hela akijifanya ni Shetta hivyo Promota amekuja kushtuka mwishoni na kumpata Shetta mwenyewe ambae walielewana.
Ilibidi aondoke Dar es salaam harakaharaka kuwahi mpaka Babati ili tu asiwakasirishe mashabiki wake ambao toka mwanzo kwenye matangazo walikua wanaamini ni Shetta kweli anakwenda kwenye show.
Mkoa wa Manyara umekua na rekodi za wasanii feki wanaojitokeza na kula hela ambapo mwaka 2013 zilitokea vurugu kwenye kiwanja kimoja, vitu kuvunjwa na watu kuumizwa baada ya mashabiki kugundua waliletewa Barnaba feki.

No comments:

Post a Comment

ShareThis