Sunday, May 11, 2014

Si rahisi kwa mwanaume kugundua haya kwa mpenzi wake.




df
Mara nyingi imekuwa ngumu kwa wanaume kungundua mabadiliko ya wapenzi wao ikiwemo mambo haya kadhaa.....

Rangi mpya ya kucha
Ni mara chache sana utakuta mwanaume huwa anagundua kwamba leo umeweka rangi tofauti ya kucha au umeweka nzuri,kwa asilimia kubwa ya wanaume,ni nadra sana kushtukia kuwa leo kuna kitu tofauti kwa mpenziye haswa tukiongelea kuhusu rangi za kucha zako za miguu au za mikono,haijalishi mpenzi wake ametumia muda gani kujaribu kutengeneza kucha zake ili apendeze au ametumia pesa ngapi kutengeneza kucha,ila most men wont even notice all of that,labda unaweza sema ni jinsi wanaume walivyoumbwa kwa kile kutoweza kujua tofauti ya rangi vizuri.

Usipopaka make-up
Mara nyingi kwa mwanamke asipopaka make up,especially ukikutana na mtu ambaye huwa mnakonana mara kwa mara, anaweza kukuuliza ,ni nini tatizo,au maswali yakizushi kama mbona leo unaonekana umepooza,vitu kama hivyo,nadhani asilimia kubwa ya wanawake wameshawahi kuulizwa maswali ya kizushi kama hayo siku ambayo wanatoka bila kupaka make-up,ukweli ni kwamba asilimia chache sana ya wanaume wanauwezo wakugundua kuwa mpenzi wake amepaka make up au la!.

Kutonyoa nywele za miguuni
Ni kweli kuwa wanawake wengi hutumia muda wao mwingi kuhakikisha kuwa wananyoa vinyweleo vya miguuni,ili kuongeza urembo zaidi na kufanya aina zote za massage,ila kwa wanaume kugundua kuwa ,leo mpenziye hajanyoa vinyweleo vya miguuni ni nadra sana kutokea,asilimia kubwa wanaweza wasiwe na ufahamu hata kama huwa unanyoa hivyo vinyweleo.

Pochi mpya
Kwa wanaume wengi kwao Pochi ni pochi tu,na kama hujagundua hili ni kuwa pale tu unapobadili size ya pochi,labda leo umebeba pochi kubwa na kesho umebeba ndogo, ndio utakuta ni rahisi kugundua,tena hiyo hutokea mara chache sana,ila kwa upande wa pochi mpya,?si rahisi kabisa kuweza kugundua.hata kama amekariri aina zako zote za pochi ulizonazo,labda tu umdokeze kuwa kama kuna kitu tofauti leo,ila apart from that,ni bahati sana umkute mwanaume anajua hilo,labda ujifanye umesahau price tag ndio agundue.

Kuvaa Hereni mpya
Asilimia kubwa ya wanaume kwa hili ni vigumu sana kugundua,najua wanawake wengi hujitahidi kubadili hereni mbali mbali za aina tofauti ,ila hapa bila ya kuuliza kama umependeza!, sidhani kama kuna mwanaume anayeweza ku-notice changes,na kama yupo ni wachache sana,mara nyingi kutiokea kama mwanamke ambae hana kabisa tabia ya kuvaa hereni,siku akiamua kuvaa hapo kuna uwezekano wakugundua.



No comments:

Post a Comment

ShareThis