Saturday, August 17, 2013

Chris Brown ahukumiwa saa 1,000 za kazi za kijamii zikiwemo za kusafisha mazingira

Chris Brown amehukumiwa upya kufanya kazi mbalimbali za kijamii kwa saa 1,000. Hukumu hiyo imetolewa jana na jaji wa Los Angeles, baada ya muimbaji huyo kwenda mahakamani jana na imetokana na kuwepo mapungufu mengi katika kazi alizotakiwa kufanya kulingana na probation aliyokuwa nayo.
rs_560x415-130816161945-1024.brown.ls.81613_copy Chris akiwa mahakamani

Katika hukumu hiyo, Chris atatakiwa kufanya kazi mbalimbali zikiwemo kusafisha mazingira na kazi zingine atakazopewa na idara ya probation.
brezy Suruali haikai kiunoni
Brown alihudhuria makahamani akiwa amevalia shati jeupe na suti nyeusi na alionekana mwenye hasira kibao huku wakati mmoja akisikika kwa sauti akimwambia wakili wake, Mark Geragos, “I understand. I understand. I am going to say whatever I want to. It’s how I feel. I don’t care.”
Mama yake Joyce Hawkins naye alikuwepo mahakamani.

No comments:

Post a Comment

ShareThis