Saturday, August 17, 2013

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Afungua Semina ya Fursa kwa vijana mkoani humo iliohudhuriwa na wanamuziki mbali mbali wa Bongo fleva.



Mkuu mkoa wa Kigoma,Kanali Mstaafu,Mh Issa Machibya akizungumza machache wakati wa ufunguzi wa Semina ya Fursa kwa vijana zinazopatikana ndani ya mkoa wa Kigoma na kwingineko,mapema leo asubuhi.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group ambao ndio waratibu wa tamasha kubwa la burudani hapa nchini la Fiesta 2013,
imehudhuriwa na vijana mbalimbali kutoka kila pembe ya mkoa huo wakiwemo na wasanii mbalimbali maarufu kutoka jijini Dar,ambao wanatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo jioni ya leo kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.Aidha katika Semina hiyo ya Fursa,baadhi ya vijana wengi walionekana kuvutiwa kwa kiasi kikubwa kwa yaliyokuwa yakizungumziwa,ikiwemo suala la ujasiliamali.
 Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akimkaribisha mgeni rasmi wa semina hiyo,Mh Issa Machibya mapema leo asubuhi,kwenye ukumbi wa Kibo Peak,uliopo Kigoma mjini,kulia kwake ni msanii mahiri wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto ambae pia likuwa ni mmoja wa watoa mada kuhusiana na suala zima la Fursa.Semina hiyo imewashirikisha wadau mbalimbali,wakiwemo NSSF,Wasanii wa Bongofleva,wakazi  wajasiliamali mbalimbali ndani ya mji wa Kigoma.
 Pichani juu ni baadhi ya Wasanii wa Bongofleva na wadau wengine wakiwemo wakazi wa Kigoma wakisiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo kuhusiana na fursa mbalimbali. 
 Sehemu ya Meza kuu ikishangilia jambo,kutoka kushoto ni Kaimu Meneja wa NSSF mkoani Kigoma,Bwa.Said Abdallah,Mkuu wa Wilaya ya Uvinza ambae alikaimu pia nafasi ya Mkuu wa wilaya ya Kigoma mjini,Mh.Khadija Nyembo,Mkuu wa Mkoa,Mh.Issa Machibya,Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji kutoka  Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,Msanii Mrisho Mpoto (haonekani) pamoja na msanii wa muziki wa kizazi kipya,ajulikanae kwa jina la kisanii AY.
 Baadhi ya Wasanii wa bongofleva ambao wanatarajiwa kutumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika,wakitambulishwa kwa wakazi wa Kigoma,wakati wa kuanza kwa semina ya Fursa iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Kibo Peak mjini humo.
 Mkali wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akifafanua jambo mbele ya wakazi mbalimbali wa mji wa kigoma,alipokuwa akiielezea mada mojawapo iliyohusiana na fursa mbalimbali zilizomo ndani ya mji huo na wakazi wake.
Baadhi akina mama walioshiriki semina hiyo wakijadiliana jambo huku wakinukuu baadhi vipengele vilivyowagusa kwa namna moja ama nyingine.

No comments:

Post a Comment

ShareThis