Friday, November 15, 2013

Audio: Fid Q na Joh Makini watoa sababu za kutokuwa na mixtapes, watoa tofauti ya mixtape na albam


Wakati ambapo suala la wasanii wa hip hop nchini kuachia mixtapes limekuwa kama fashion kwa sasa, kuna dalili nyingi kuwa wengi wa wasanii hao hawana ufahamu wa kutosha juu ya chimbuko la mixtape na tofauti kati ya mixtape na albam.
Mwana FA, Fid Q, AY, Arthur na mshikaji
Fid Q
Fareed Kubanda aka Ngosha na Joh Makini wamejaribu kuchambua kwa upeo wao tofauti ya
mixtape na albam kwenye utamaduni wa Hip Hop, na kutoa sababu za kwanini mpaka hivi sasa hawana mixtape hata moja kitaani na kama ni sahihi kufanya biashara kwa mixtape ndani ya wigo wa malalamiko ya ‘albam haziuzi’.
Fid Q akitoa maana ya mixtape, tofauti yake na Album na Street EP
Wasanii wengi wa hip hop wameshindwa kutofautisha kati ya mixtape na official street EP na official album. Mixtape inaweza ikawa labda kuna beat ya Fid Q, kuna beat ya One Incredible, kuna beat ya Nikki Mbishi, kuna beat ya Profesa Jay ndani, lakini labda hiyo mixtape ni ya labda lets say Kadigo au Young Killer.
Lakini official street EP mtu unaweza kufanya compilation zako zote we mwenyewe lakini ukaamua kwamba hii bado siyo official album hii ni street EP. Kwasababu unajua watu wengi wanasahau kuhusiana na album, albam siyo compilation of songs kwamba eti mtu unaenda kucompile tu nyimbo hizi hizi hizi, Nah lazima iwe na theme kwasababu themes are very important. Kwamfano mtu unafanya kitu kinaitwa Kitaolojia, lazima kila nyimbo iwe ime link na maswala ya mtaa na nini na vitu kama hivyo.
Sasa unajua watu wengi wanasema wanatoa album lakini ukiskiliza unaona kabisa hii ni compilation, unaelewa ambapo mimi ningewashauri labda wangeita street EP. Kwahiyo ni vitu flani ambavyo viko very complicated lakini ni hesabu ndogo tu ambazo ukizipiga unakuwa unaelewa unachomaanisha.
Kuhusu sababu za yeye kutokuwa na mixtape
Mixtape unajua waga inampa msanii ule uhuru kwamba mtu anatumia beat ya mtu yeyote akaimbia ndani na nini na nini, lakini mimi hua pia nataka kufanya mixtape but kila muda ambao nataka kufanya mixtape kile kitu ambacho nafanya kinasound too official, kwahiyo ukifanya mixtape nakuwa kama nimedisrespect sanaa yangu mwenyewe.
Kwa mfano kama watu wa mpira, mixtape ni ligi ya daraja la nne, albam daraja la kwanza, kwahiyo kila muda ambao nafikiria kwamba kiwango change cha daraja la nne, nakuwa napiga viwango vya daraja la kwanza kwahiyo nakuwa kama nimeenda daraja la nne kupoteza muda muda wangu, ndio maana mimi nakuwaga sifanyi mixtape nafanya album.
Mtazamo wa Fid juu yab ma mc wanaofanya mixtape na kuzifanyia biashara, je ni sahihi?
Ni sahihi sana kwasababu kitu kama hicho hakikuwepo zamani, ni sahihi sana mi huwa naona ndio kukua kwenyewe kwa hip hop, na inasaidia unajua mtu unapokuwa una mixtape yako unakuwa unauza inakuamsah kidogo kuhusiana na biashara kwasababu watu wenye talent ni wengi lakini wangapi ambao wanapata mkate wao wa kila siku kupitia vipaji vyao walivyonavyo. Kwahiyo na mtu unapokuwa unamiliki mixtape inakuwa inasaidia kidogo kukupa ile changamoto ya kuiangalia future yako iko wapi na sanaa yako ambayo unafanya, kwahiyo mimi nasapoti wasanii wote ambao wanakuwa wanatoa mixtape na wanajaribu ku hustle katika kujipatia mkate wao wa kila siku kwasababu ile ni njia sahihi ambayo inamsababisha mtu aone, okay mimi labda fan base yangu ni kubwa kiasi hiki au ni ndogo kiasi hiki nachotakiwa kufanya ni hiki na hiki na hiki, afu kumbuka unajua usanii wa mtu haukamiliki bila kuwa atleast na album lakini unapokuwa na mixtape inakuwa ni step ya kwanza.
Joh-makini
Joh Makini
Joh Makini akizungumzia maana ya mixtape na chimbuko lake
Kwanza lazima ufuatilie chimbuko la mixtape nini chanzo cha mixtape, mixtape unajua ilianza kutokana na unajua kwa America huwezi kufanya album kama hauko kwenye recording company kubwa, kwahiyo wasanii ni wengi na ma mc wengi wanataka kufanya vitu kila siku watu wanakuja na idea mpya. Kupata recording label ni ngumu na kuingia kwenye rotation ya kufanya album wakati mwingine ni ishu ukitaka kupata hizo deals, kwahiyo watu wakagubdua kwamba ili kusudi tusiendelee kuskilizia wakati tunasubiri kupata recording deal kubwa za kufanya albam, lazima tuwe na kitu cha kufanya ambacho kitakuwa kinatufanya tuendelee kuwa kwenye mzunguko wa kazi ndo hapo ilipozaliwa mixtape…yaani mixtape ni kama albam isiyo rasmi.

Joh akizungumiza sababu za yeye kutokuwa na mixtape

Kama una advantage na uwezo wa kufanya albam, huna sababu ya kufanya mixtape, halafu kama una material unajua mixtapes na albam ni two different materials, kuna watu material zao ni mixtapes hata akiamua kufanya album serious ukiendelea kukagua utagundua sio albam ni mixtapes, lakini sisi tuna materials za albam. Ukiangalia mixtapes ni kitu flani ambacho mtu anaweza akachukua beat ya mtu flani akapiga michano amecopy copy flani kuonesha ujuzi wa rap na vitu kama hivyo. Unaona mtu anaweza kufanya mixtape asitengeneze hata beat moja unajua akachukua tu beat za watu na hiyo inaruhusiwa kwenye hip hop, kwahiyo mixtape siyo kitu kibaya, ni kitu kizuri kwasababu kinakufanya uendelee kuwa kwenye rotation ya kile ambacho unakifanya daily, umenielewa lakini kama una material za kufanya albam unatakiwa ufanye albam, Weusi tunakuwa hatufanyi sana mixtapes, acha Weusi mimi Joh Makini sijawahi kufanya mixtape mimi niliwahi kufanya album ya kwanza mwaka 2007 na kitakachofata kingine ni album kwasababu material yangu yote yanapaswa kuingia ndani ya album ni albums tu na video sio mixtapes material.
Mtazamo wa Joh kuhusu ma mc kufanya mixtapes na kuzifanyia biashara
Mi nadhani hiyo ya kudownlaod for free kwenye Internet ambayo tunafanya huku bongo ni piracy, kule Marekani hata mixtapes zinauzwa wanaingia deal na watu ambao wana hizo network za kwenye intenet, kwahiyo unakuta ukidownload kwenye itunes kule unalipia ukilipia yule msanii inamfikia lakini hii ya kudownload ambayo tunafanya huku bongo ni piracy, hata kule Marekani mixtapes zinauzwa vizuri tu na tena zingine waga zinavunja rekodi za mauzo kabisa unasikia wimbo flani uko kwenye mixtape flani na umevunja rekodi ya mauzo kuliko hata album kadhaa za watu baadhi, kwahiyo hata kule Marekani mixtapes bado ni biashara na watu wanauza vilevile.
(Kibongo bongo) mi naona ni biashara na nashukuru kuona inaendelea kufanya mzunguko wa rap unakuwa mzuri na ma mc wanakuwa na kitu cha kufanya, unajua kwasababu ni ngumu kufanya albam, na ni ngumu kupata deal nzuri ya kusambaza albam, kwa kipindi hiki wakati watu wanasubiri kutengeneza hiyo michongo sio vibaya wakifanya mixtape ni moja kati ya tamaduni za ki hip hop. Kwahiyo sio kitu kibaya kufanya mixtape kama una nafasi na una hizo mixtape material, lakini siyo lazima kufanya mixtape kama huna mixtapes material una album material kama mi navyofanya.
Fid Q na Joh Makini walifunguka kuhusu mixtapes kupitia Showtime ya Radio Free Africa Mwanza wiki hii na mtangazaji Renatus Kiluvia aka Bizzo.
Msikilize Fid Q akizungumzia kuhusu mixtape

Msikilize Joh Makini akizungumzia mixtape



No comments:

Post a Comment

ShareThis