Friday, November 8, 2013

Rais Kikwete asema Tanzania haina mpango wa kujitoa EAC


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema Tanzania haina mpango wa kujitoa kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki licha ya Kenya, Uganda na Rwanda kuonesha dalili za kuitenga.
Jakaya Kikwete, president of Tanzania, answers questions at a press conference at the United Nations (UN) building in Addis Ababa, Ethiopia, during the 12th African Union (AU) Summit.
Akilihutibia bunge jana kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010, Rais Kikwete alisema Tanzania ni nchi mwanachama mtiifu na
kamwe haiwezi kujitoa.
“Napenda kuwahakikisha wabunge kuwa hatuna mpango wa kutoka katika Jumuiya,”alisema Kikwete.
“Tupo na tutaendelea kuwepo. Tanzania haijafanya jambo lolote baya dhidi ya Jumuiya, au nchi yeyote mwanachama. Kama kuna ushahidi watuambie tu. Na ukweli ni kwamba sisi Tanzania ni wanachama wavumilivu. Sisi ni watiifu na waaminifu kwa Jumuiya.”

Rais Kikwete alisema kauli ya baadhi ya viongozi wa nchi hizo kuwa wanaendelea kufanya mikutano bila kuialika Tanzania kwa madai kuwa haipo tayari, si ya ukweli.

“Hatujaalikwa, kama hatujaalikwa kwanini waseme wao ndio the willing na sisi ndio the unwilling. Madai haya hayana ukweli, ni vyema waseme ukweli tu. Kama walitualika, tukakataa ndio wanaweza kusema hivyo, lakini sijapata mwaliko hata mmoja.”

Aliongeza kuwa madai kuwa Tanzania ni kikwazo kwa nchi zingine na kwamba inawachelewesha wengine kupiga hatua za haraka kimaendeleo hayana ukweli wowote.

Alisema msimamo wa Tanzania kuhusu kuharakisha shirikisho la Jumuiya ya Afrika Mashariki, masuala ya ardhi, ajira na uhamiaji ndio yanaleta kile alichokiita ‘hisia zisizo sahihi’.


No comments:

Post a Comment

ShareThis