Sunday, April 13, 2014

Shetta asema anaendelea vizuri kidogo baada ya kupata ajali ya gari mkoani Babati


Msanii wa muziki Shetta amesema anaendelea vizuri baada ya kupata ajali ya gari hapo juzi maeneo ya Minjingu akielekea Babati kwa ajili ya kufanya show.
page
Shetta na gari aina ya Naoh aliyopata nayo ajali
Akizungumza na wana bongo5 leo,Shetta,amesema kuwa mpaka sasa bado yupo Babati na
ameshapata huduma ya kwanza ingawa bado ajisikii vizuri
“Namshuru mungu naendelea vizuri,nipo Babati mjini,nimepata uduma ya kwanza ila bado siko vizuri sana,naomba tuongee baadae”Alisema Shetta.
Shetta alipata ajali wakati anaelekea Babati na gari ya aina ya Noah,jioni ya April 11 2014 baada ya gari kupinduka mara tatu wakati dereva akiwa kwenye jitihada za kumkwepa Punda.
Kwenye gari hilo, Shetta alikua na msaidizi wake pamoja na waandaaji wa show ambapo hakuna aliepoteza maisha isipokua majeraha madogomadogo huku yeye mwenyewe akiumia kichwani na mguuni.
“nashukuru mungu nimetoka salama kweli mungu mkubwa mana nilijua leo ndo mwisho wangu mana ajali ni mbayaaa sanaaaaa…… thnx woteee mlionipa pole tupo pa1.”Shetta alisema baada kusurika na ajali hiyo.


Credit:Bongo5

No comments:

Post a Comment

ShareThis