Sunday, May 11, 2014

Maneno ya Diamond Platnumz kuhusu kuvuja kwa nyimbo yake

Hii leo kulikua na purukushani kwenye blogs kuitangaza nyimbo mpya ya Diamond iitwayo
Kitorondo. Kama ulipata muda kuisikiliza nyimbo hiyo ni wazi ungejua kwamba nyimbo hiyo imevuja, Kwanza Diamond hawezi kutoa nyimbo bila kuitangaza na maandalizi ya ukweli na pia ni quality ya nyimbo yenyewe. Na haya ni maneno aliyosema Diamond Patnumz kuhusiana na kuvuja kwa nyimbo hiyo
Moja ya nyimbo zangu ambazo ziko store hazija toka nimeikuta mtandaoni na sijui imefikaje, tena ikiwa kwenye mfumo wa Voicenote, yaani haina quality kabisaa… Tafadhari, kwa yoyote atakaeipata Asiitumie kwenye media ama hadhara, kwasababu Haijatoka na haiko Qualified….
Diamond Platnumz



No comments:

Post a Comment

ShareThis